Full-Width Version (true/false)


RIYAMA ALLY ANYOOSHA MANENO KUHUSU WEMA SEPETU


Msanii wa filamu Bongo, Riyama Ally amesema hakukuwa na ugomvi wowote kati yake na Wema Sepetu kama ilivyokuwa ikielezwa hapo awali.

Muigizaji huyo ameeleza kuwa si Wema tu bali msanii yeyote katika tasnia hiyo hana ugomvi naye kwani si kitu kizuri katika kazi.

“Sina ugomvi na msanii yeyote hasa Wema ndio maana hata pale airport tulizungumza na kupiga picha pamoja. Wema nimemzidi umri ni mdogo wangu na tunaheshimiana katika kazi sina ugomvi naye,” Riyama ameiambia Bongo5.

“Sisi ni familia tunapokuwa na ugomvi na chuki tunakuwa tumejiwekea vizingiti au ukuta katika kazi zetu. Kesho na keshokutwa tutaambiwa tufanye kazi pamoja tutashindwa kwa ajili ya ugomvi,” amesisitiza.

Ameongeza kuwa kwa kuelewa hilo kumemfanya kupenda kujishusha zaidi kuliko kujikweza ili aweze kuelewana na kila mtu na kuweza kufanya kazi na kila mtu.

Chanzo cha taarifa za kutoelewana kwa Riyama Ally na Wema Sepetu kulidaiwa ni baada ya Wema kushinda tuzo mbili za Sinema Zetu International Film Festival Awards (SZIFF) Aprili Mosi mwaka huu, kitu ambacho Riyama amesema hapendi kukizungumza mara kwa mara.

No comments

Powered by Blogger.