Full-Width Version (true/false)


Sababu ya Abramovich kupewa uraia wa Israel

Moja ya stori ya uifahamu leo May 29, 2018 ni kumhusu miliki wa Klabu ya Chelsea, Roman Abramovich amepewa uraia wa Israeli baada ya Uingereza alikowekeza kushindwa kumpatia Viza.

Abramovich ameshindwa kupewa viza kutokana na mzozo wa kidiplomasia kati ya taifa la Uingereza na Urusi, na yeye ana uraia wa Urusi.
Imeelezwa kuwa imekuwa rahisi kwa mfanyabiashara kupata uraia wa Israeli kutokana na kuwa na asili ya taifa hilo. Amepewa uraia huo kupitia sheria inayowapa kipaumbele watu wenye asili ya Israeli wanaotaka kurejea nchini kwao.

Serikali ya Uingereza haitokuwa na kipingamizi kwa mfanyabiashara huyo kwakuwa ataomba viza kama raia wa Israel. Abramovich amenunua jumba la kifahari katika mji wa Tel Aviv.

No comments

Powered by Blogger.