Sababu ya Matheo Anthony kutaka kuondoka Yanga hii hapa...
Mshambuliaji
wa Yanga, Matheo Antony ameonyesha hali ya kujiondoa kikosini hapo
akitaka timu yake impe ruhusa ya kuchagua timu ili aende kucheza hata
kwa mkopo ili aonyeshe ubora wake.
Matheo
amedumu Yanga kwa zaidi ya misimu minne huku akiandamwa na majeraha
yaliyomfanya kukosa namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo
kilichoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi.
Matheo
alisema kuwa mkataba wake na Yanga unatarajia kumalizika mwishoni mwa
msimu ujao, hivyo kwa kuwa bado ni mchezaji halali wa Yanga angependa
apewe nafasi ya kucheza hata kwa mkopo katika timu nyingine ili
akaonyeshe uwezo wake zaidi.
“Natamani
sana katika usajili huu viongozi wangu wanipe nafasi ya kujaribu
kucheza nje ya kikosi changu hata kwa mkopo ili nikaangalie changamoto
mpya kwani yawezekana hapa nakosa nafasi kutokana na kuwepo kwa
mastraika wengi wazuri.
“Nasubiria
watakapoanza tu kusajili niombe hilo kama nitakubaliwa basi ningependa
zaidi niende Lipuli FC ya Iringa, kwani pale naamini nina uwezo mkubwa
wa kupata nafasi hasa ukilinganisha washambuliaji wake wengi naona wana
uwezo kama wangu tu,” alisema Matheo.
No comments