Full-Width Version (true/false)


Sababu za Alikiba kuitosa kolabo na Ne-Yo, Man Walter aeleza A-Z

 
Producer anayedondosha hit baada ya hit kutoka kwa Alikiba, Man Walter amefunguka sababu ya muimbaji huyo kuachana na mpango wa kumshirikisha Ne-Yo katika ngoma yake ya Seduce Me.


Man Walter amesema tayari mipango yote ya kufanya kolabo hiyo ilikuwa imekamilika ikiwa ni pamoja na kumtumia vocal ila baadaye walikuja kuona muimbaji huyo alikuwa na kolabo nyingi na wasanii kutoka Afrika.

“Nilipigiwa simu nikaambiwa Kiba anafanya na Ne-Yo, nikaanza kutafuta biti nikapata biti ila nikasema mbona ni danso kama Miss Independent ya Ne-Yo, nikasema niitoboe kidogo nipate kitu ambacho naweza kutambulisha vitu vyetu vya Kiafrika, tukapata kitu kama kile, Kiba aliifurahi,” amesema.

“Tukatuma pia kwa Ne-Yo kulikuwa kuna mazungumzo yanaendelea na kukamtumia zile sauti but sijui nini kilitokea katika maamuzi labda pengine Kiba aliona Ne-Yo kwa wakati ule alikuwa na project nyingi za kufanya na wanamuziki wa Afrika, watu wasije wakaona kama tumeadandia kolabo ya bure, tukafanya maamuzi, tuachane nayo,” Man Walter ameiambia All Access ya Clouds TV.

Utakumbuka Ne-Yo kutoka nchini Marekani ameshafanya kolabo na msanii mmoja kutoka Tanzania, Diamond Platnumz ambaye mwaka 2017 walidondosha wimbo uitwao Marry You. Alikiba ambaye kwa sasa anatamba na ngoma inayokwenda kwa jina Mvumo wa Radi nayo ilikuwa katika mipango ya kushirikishwa Fally Ipupa kutokea Congo, hata hivyo nalo liliwekwa kando.

No comments

Powered by Blogger.