Full-Width Version (true/false)


Sababu za ngoma mpya ya Alikiba ‘Mvumo wa Radi’ kutokuwepo Vevo

Meneja wa Alikiba, Seven Mosha ameeleza ni kwanini wimbo mpya wa muimbaji huyo ‘Mvumo wa Radi’ unapatikana YouTube na sio Vevo.
Mosha ameiambia Clouds Fm kuwa wimbo huo umetoka kwa ajili ya kutangaza bidhaa yake mpya energy drink, Mo Faya na wimbo huo umelenga soko la Afrika Mashariki.

“Ni wimbo ambao umetoka kutambulisha product yake for the first time maana malengo yetu ni kutengeneza awareness halafu namba mbili tunatafuta distributors, kama alivyosema malengo yake ni East Africa akaamua kabisa lets introduce East Africa song maana ndio key market ya Mo Faya,” amesema.

Nyimbo za Alikiba ambazo zinapatika Vevo kwa sasa ni pamoja na Seduce Me na Aje Remix.

Seven Mosha ameongeza kuwa Sonny Music International wamekubali hicho anachofanya Alikiba kwa sasa ila nyimbo zote zinazokuwa chini ya label hiyo zinawekwa Vevo lakini project binafsi za Alikiba zinawekwa YouTube.

No comments

Powered by Blogger.