Full-Width Version (true/false)


Sadio Mane agawa jezi 300 kijijini kwao Senegal

Mshambuliaji Sadio Mane amenunua jezi 300 na kuzituma kijijini kwao nchini Senegal.

Jezi hizo za Liverpool zitavaliwa kesho wakati Liverpool ikiivaa Madrid katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa jijini Kiev.


Mane amesema amefanya hivyo baada ya kusikia katika kijiji alichozaliwa cha Bambali, kuna watu wengi wameamua kuhama timu kadhaa na kuiunga mkono Liverpool kesho.


Mane amekumbusha kwa kusema hata yeye, aliwahi kuwa shabiki mkubwa wa FC Barcelona kabla ya kuhamishia mapenzi yake Liverpool.

No comments

Powered by Blogger.