Full-Width Version (true/false)


Sahau kulipia king’amuzi, fainali ya UEFA kati ya Real Madrid na Liverpool kuoneshwa mubashara YouTube

Kama bado unaumiza kichwa jinsi gani utatazama fainali ya klabu bingwa barani Ulaya ile hali bado hujalipia king’amuzi chako nyumbani. Ondoa mawazo hayo kwani mchezo huo wa fainali kati ya Real Madrid na Liverpool utarushwa live kwenye mtandao wa YouTube.


Fainali hizo zitaonesha Live kwenye Channel ya YouTube ya BT Sports inayomilikiwa na kampuni ya BT Group yenye makao makuu yake nchini Uingereza.

Kwa mujibu wa mtandao wa BT Sports wameeleza kuwa hii itakuwa kwa simu au kifaa chochote chenye uwezo wa kucheza ukubwa wa 4k .

Lengo hasa la BT Sports kufanya hivyo ni kusaidia wapenzi wa soka ambao wanatumia gharama kubwa kutazama mpira.

Fainali ya UEFA kati ya Real Madrid na Liverpool itapigwa Tarehe 26, Mwezi huu kunako dimba la NSC Olimpiyskiy mjini Kiev.

No comments

Powered by Blogger.