Full-Width Version (true/false)


Sakata la sukari na mafuta lamkumbusha Zitto Bunge la tisa

 
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amempongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai baada ya kuitaka serikali itoe majibu ya kina kuhusu kupanda bei ya sukari.

Zitto ametaka na suala la mafuta litazamwe kwa muktadha wa wakulima wa Mawese na Alizeti.

“Namna ambavyo Spika Ndugai amesimamia suala la Majibu ya Serikali kuhusu Kadhia ya Sukari na Mafuta ya Uto (kula) inanikumbusha Bunge la Tisa. Ndugai sasa ameanza kuweka ‘legacy’ yake. Aendelee hivi. MUHIMU: Suala la Mafuta litazamwe kwa muktadha wa Wakulima wa Mawese na Alizeti,” ameandika Zitto kupitia ukurasa wake wa Twitter.


Hata hivyo jana, Bungeni Mjini Dodoma, Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, alishindwa kutoa majibu ya serikali baada ya Mbunge wa Mpendae, Salim Turky (CCM), kuihoji serikali, Kwanini sukari imekuwa ikiuzwa bei ghali upande wa Tanzania Bara tofauti na ilivyo Zanzibar.

Jana, Spika Ndugai aliingilia kati suala hilo la kupanda kwa bei ya sukari na kusema kuwa “suala hili ni la Msingi sana kwa wananchi wa Tanzania na kwakweli halijapata majibu kwahiyo tutalipanga tena kwenye maswali ya wiki ijayo ili serikali itupe majibu ya kina linapaswa kutolewa majibu ya kina na serikali.”

No comments

Powered by Blogger.