Full-Width Version (true/false)


Salaamba kaula,unaambiwa mshahara wake ni noma

 
IMEFAHAMIKA kuwa mshambuliaji tegemeo wa Lipuli FC, Adam Salamba, atapokea mshahara wa shilin­gi milioni mbili kwa kipindi cha miaka miwili ambacho ataichezea Simba, ambao ni sawa na shilingi milioni 48 kwa mkataba wake wote.


Mshambuliaji huyo alisaini mkataba huo wa miaka miwili juzi akitokea Lipuli ambayo ilimu­uza baada ya Yanga na Azam FC kushindwa kuinasa saini ya nyota huyo wa kupachika mabao.


Salamba aliyemaliza msimu na mabao sita, anatarajia kuungana na mshambuliaji wa Majimaji FC ya Ruvuma, Marcel Boniventure aliyefunga mabao 14 kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara.


Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, Salamba alisaini mkataba huo wa miaka miwili kwa dau la shilingi milioni 40.


Mtoa taarifa huyo alisema, katika dau hilo la usajili lililotolewa na Simba, shilingi milioni 25 zilik­wenda kwa timu yake ya zamani ya Lipuli, iliyommiliki kwa ajili ya kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja wa kuendelea kuichezea timu hiyo.


“Uongozi wa Lipuli ni lazima unu­faike na mauzo ya Salamba, kama unavyofahamu mchezaji alikuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuichezea Lipuli.


“Hivyo, kabla ya mchezaji huyo kusaini mkataba, yalifanyika mazungumzo kati ya sisi timu tunaommiliki mchezaji, mchezaji mwenyewe na uongozi wa Lipuli kwa ajili ya kukubaliana baadhi ya vitu ikiwemo kupata sehemu ya fedha kwa ajili ya kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja katika dau hilo la usajili.


“Uzuri ni kwamba hayo yote yalifanyika na kufikia muafa­ka kuwa sisi Lipuli tupatiwe shilingi milioni 25 za kusi­tisha mkataba wa Salamba pamoja na makubaliano mengine ya bin­afsi kati ya mche­zaji na uongozi wa Simba.


“Salamba atanufaika na mshahara huo atakaokuwa anaupata Simba, kwani akiwa Lipuli alikuwa analipwa mshahara wa Sh 500,000, pia Simba wam­empatia usafiri wa kutembelea ambao ameshak­abidhiwa,” alisema mtoa taarifa huyo.


Alipotafutwa Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Simba, Said Tully kuzun­gumzia hilo alisema: “Dau la usajili la mchezaji ni siri kati ya mchezaji na uon­gozi wa timu am­bayo yapo kwenye mkataba.


“Timu yetu ipo kwenye mikakati mikubwa ya usa­jili na zipo sehemu ambazo zinahitaji kufanyiwa maboresho kwa mujibu wa ripoti ya kocha ambayo ni safu ya ushambuliaji ambayo tumeanza nayo.”

No comments

Powered by Blogger.