Full-Width Version (true/false)


SALAH AZIDI KUWA PASUA KICHWA ULAYA, ABEBA TUZO MBILI LIVERPOOLNyota Mmisiri anayeitumikia ya Liverpool, Mohamed Salah, usiku wa kuamkia leo ameshinda tuzo mbili za klabu hiyo.

Salah ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu mzima wa timu pamoja na ya mchezaji bora wa klabu aliyechaguliwa na wachezaji wa kikosi cha Liverpool.

Mbali na tuzo hiyo, Salah pia alifanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya England kwa msimu mzima wa 2017/18.

Nyota huyo amefunga jumla ya mabao 43 katika mashindano yote huku akicheza jumla ya michezo 50. 

No comments

Powered by Blogger.