Full-Width Version (true/false)


SALAMA SALIMINI, YANGA WAKO NCHINI ALGERIA TAYARI KWA KAZI YA JUMAPILIMabingwa wa soka nchini Yanga, wametua salama nchini Algeria tayari kuivaa USM Alger, keshokutwa.

Yanga iko nchini humo tayari kuwavaa vigogo hao katika mechi yao ya kwanza ya hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Kikosi hicho mjini Algeri kimepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Omar Yusuph Mzee.

Balozi huyo ambaye ni mwanamichezo, aliwapokea na kuwasindikiza hadi hotelini na kesho, Yanga watafanya maandalizi yao ya mwisho kabla ya mechi hiyo ya keshokutwa.

No comments

Powered by Blogger.