Full-Width Version (true/false)


Samatta aamua kuwakazia UbeligNohodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta usiku wa jana ameibuka shujaa kwenye timu yake baada ya kutinga nyavuni mara mbili akiisaidia timu yake ya KRC Genk kushinda kwa mabao 4-1 dhidi ya Sporting Charleroi. 


Samatta anaonekana kurejesha makali yake baada ya kucheza bila kufunga kwa muda mrefu hadi alhamisi iliyopita alipoanza kufunga akiisaidia timu yake kutoka sare ya 1-1 na AA Gent na jana suiku kuongeza mabao mengine mawili.

Samatta amefunga mabao hayo katika dakika za 24 na 61, huku mabao mengine yakifungwa na Leandro Trossard dakika ya 34 na Dieumerci N'Dongala dakika ya 77, na bao la Sporting Charleroi likifungwa na Cristian Benavente dakika ya 31.

Jana Samatta amecheza dakika zote 90 na sasa amefikisha mabao 25 katika mechi yake ya 88 tangu nyota huyo wa Taifa Stars ajiunge na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

No comments

Powered by Blogger.