Full-Width Version (true/false)


Saudi Arabia kuwaachia wafungwa 1000 wa Ethiopia

Waziri Mkuu wa Ethiopea Abiy Ahmed amesema kuwa amefanikiwa kuomba wafungwa 1000 wa Ethiopia waliofungwa Saudi Arabia kuachiwa huru.

Hayo waziri huyo ameyazungumza baada ya ziara yake nchini Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa habari,ndege iliyokuwa imebeba wafungwa 690 ilitua Addis Ababa muda mchache tu badaa ya ndege ya waziri mkuu kufika.

Vilevile Ahmed amemuomba Mwanamfalme wa Saudi Arabia kumuachia huru mfanyabiashara maarufu aliyezaliwa Ethiopea na sasa ni raia wa Saudi Arabia ,Mohammed Hussein al-Amoudi.

Mohammed Hussein al-Amoudi ametoa ajira kwa zaidi ya raia 70,000 nchini Ethiopia.

"Natumaini ataachiwa hivi karibuni",alisema waziri Ahmed.

Mohammed Hussein al-Amoudi alikamatwa pamoja na wanawafalme na wafanyabiashara wengine maarufu wakati mwanamfalme wa Saudi Arabia akipambana na rushwa.

No comments

Powered by Blogger.