Full-Width Version (true/false)


SeeBait Inasikitisha! Muuguzi Amefariki kwa Ugonjwa wa Ebola Wakati Chanjo Inatolewa

Inasikitisha! Muuguzi Amefariki kwa Ugonjwa wa Ebola Wakati Chanjo Inatolewa
Chanjo ya Ebola imeanza kutolewa nchini DRC huku muuguzi mmoja akiripotiwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo katika mji wa Bikoro, kaskazini magharibi mwa taifa hilo na kuongeza idadi ya waliokufa kutokana na mlipuko wa Ebola kufikia 27.

Mkuu wa shirika la Afya Duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema mjini Geneva katika mkutano wa kila mwaka wa WHO unaohudhuriwa na nchi wanachama 190 kuwa anafurahi kwamba chanjo hiyo imeanza kutolewa na amefurahishwa na hatua za dharura za kimataifa zilizochukuliwa kuukabili.

No comments

Powered by Blogger.