Full-Width Version (true/false)


Serena Williams aanzisha brand yake ya nguo

 Mchezaji tennis maarufu nchini Marekani Serena Williams ameamua kuja na ujio mpya wa brand yake ya nguo “Serena” ambazo nguo hizo zitauzwa kwa njia ya mtandao na ameamua kushare taarifa hizo za furaha kupitia ukurasa wake wa Instagram.


Serena Williams ameandika “Wanasema maisha ni kuhusu muda , nimejifunza kitu nikiwa na umri wa miaka 18 nilivyoamua kucheza tennis kwasababu nilitaka kwenda shule ya mitindo , wengi walipinga maamuzi yangu lakini nilijua nina mapenzi kwenye vitu viwili ambavyo ni tennis na mitindo na nilitafuta muda kuyatimiza yote”


“Baada ya miaka 15 ya mwanzo na watu wengi kwenye mitindo kuniambia siwezi ilinipa nguvu kufanya kazi kwa bidii, na matokeo yake nikagundua kuwa nijiwekeza mwenyewe na nilijiruhusu kujiamini mwenyewe ili kufikia ndoto zangu”


“Leo hii nafurahia kuzindua Serena  kama duka moja wapo la mtandaoni usiache kujiamini wewe ni wa thamani”


No comments

Powered by Blogger.