Full-Width Version (true/false)


Serikali kuhakikisha Watanzania wanaajiriwa katika maeneo nyetiSerikali imesema kuwa itahakikisha Watanzania wanapata fursa ya kwanza kuajiriwa katika maeneo yote nyeti kama vile bandari, uwanja wa Ndege na kwenye mipaka ya nchi ili kusiwepo na jambo lolote la kuvunjika kwa amani ya nchi.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Bungeni, Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum, Leah Komanya juu ya Serikali kuchunguza na kuchukua hatua ikiwa kuna wafanyakazi wa kigeni ambao wameajiriwa katika maeneo nyeti kama vile viwanja vya ndege, bandari na kwenye mipaka ya nchi.

Aidha Majaliwa amesema Serikali imeratibu vizuri sana suala la ajira nchinia na ajira zitakazotolewa kwa wageni ni kwa nafasi zile za wataalamu ambao Watanzania hawawezi.

No comments

Powered by Blogger.