Full-Width Version (true/false)


Serikali kushughulikia suala la kupima Ukimwi kwa kutumia kipimo cha mate

Serikali imesema kuwa wamemuandikia barua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili aweze kuleta mabadiliko ya sheria ili iweze kuruhusiwa mtu kujipima Ukimwi mwenyewe na kutumia kipimo cha mate.Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameyaeleza hayo, leo Mei 31 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge Masoud aliyehoji,
Kwa kuwa hali ya Maambukizi katika jiji la Dodoma unaongezeka kwa kasi sana na kwa kuwa katika baadhi ya Nchi duniani wanatumia njia Mbadala ile ya kuweza kutumia mate kuweza kutambua wale waathirika wa VVU, naomba serikali ituambie ina mkakati gani wa ziada kuleta mkakati huu mpya wakuwatambua waliopata athari hii VVU kwakutumia njia ya kutumia mate na hasa tukianzia Mkao huu wa Dodoma?
“Lakini saula njia mbalimbali za kupima ni kweli tumekuwa na changamoto ya kuwapata watu kupima hasa wanaume tumeona na tumeona njia ambayo itaweza kusaidia wanaume kupima Ukimwi ni njia ya mtu kujipima mwenyewe na jana tulikuwa na Waziri Mkuu na moja ya kifaa ambacho tutakitumia,” amesema Ummy.

“Lakini Sheria kidogo zinatukwaza kupima tutatumia kipimo katika facilities cha kujipima mwenyewe haiwezekani, kwahiyo tumemuandikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili aweze kuleta mabadiliko madogo ya sheria ili iweze kuruhusiwa kwa mtu kujipima ikiwemo kutumia kipimo cha mate ambapo kwa dakika 15 utaweza kujua kama una Maambukizi au hapana na tunaamini mtu akishajipima mwenyewe na kujiona kwamba ana maambukizi itakuwa ni kichocheo cha kwenda kwenye kituo cha afya ili aweze kudhibitika ili aweze kuingizwa kwenye mpango wa dawa,” ameongeza.

Aidha Ummy amesema kuwa dawa za HIV zipo kwa asilimia 100 changamoto watu waende kupima na kwasasa Ukimwi sio sentensi ya kifo.

No comments

Powered by Blogger.