Serikali yabanwa Bungeni migogoro ya wakulima na wafugaji
Kamati
ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imeitaka Serikali kuwasilisha
bungeni taarifa ya Tume iliyochunguza migogoro kati ya wakulima na
wafugaji ili chombo hicho cha Dola kiweze kutekeleza wajibu wake wa
Kikatiba.
Akisoma
taarifa ya kamati hiyo leo bungeni Mei 15, 2018, Makamu Mwenyekiti wa
kamati hiyo, Dk Christine Ishengoma amesema migogoro baina ya wakulima,
wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi ina athuri uzalishaji katika
sekta ya kilimo.
Amesema migogoro hiyo imesababisha hofu, uvunjifu wa amani, vifo na uharibifu wa mali na mazingira.
Dk
Ishengoma amesema uchambuzi wa kamati umebaini migogoro ya matumizi ya
ardhi ni mtambuka hivyo suluhu yake inaweza kupatikana kupitia jitihada
za pamoja miongoni mwa sekta husika.
“Kwa
kutambua hivyo na kuzingatia malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na
wabunge bungeni ambao kimsingi ndio wawakilishi wa wananchi, yalipelekea
Serikali kuunda Tume inayohusisha wizara tano zinazohusika na ardhi,”
amesema Dk Ishengoma.
“Kamati
inashauri ni vyema taarifa ya Tume hiyo ikawasilishwa bungeni ili Bunge
liweze kutekeleza wajibu wake wa kuishauri Serikali.”
Dk
Ishongoma amesema Serikali iongeze kasi ya kutekeleza kwa vitendo
Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi kama ilivyoainishwa kwenye Sheria ya
Ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 1999, pamoja na kuhuisha sheria
nyingine zinazosimamia matumizi, umiliki, uhifadhi ili kuwa na uelewa wa
pamoja kuhusu ardhi.
No comments