Full-Width Version (true/false)


Serikali yakiri watu 26 kuuwawaSerikali ya Burundi imesema kuwa watu 26 wameuawa wakati wa shambulio Kaskazini Magharibi mwa taifa hilo na watu wanaodhaniwa kuwa ni magaidi. 
Ghasia hizo zimetokea siku kadhaa kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni iliokumbwa na utata ambayo huenda ikaongeza muda wa kutawala wa rais wa taifa hilo.

Kwa mujibu  wa BBC, Waziri wa Usalama nchini humo Alain Guillaume Bunyoni amesema kuwa wale waliotekeleza shambulio hilo walikuwa ni magaidi kutoka nchini jirani ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Amesema baadhi ya waathiriwa waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini ambapo wanatibiwa. na kuongezea kuwa mazungumzo yanaendelea na mamlaka ya DRC kwa lengo la kuwakamata washukiwa wakamatwe.

Pamojana hayo mashuhuda wanasema kuwa washambuliaji hao waliingia nyumba baada ya nyumba usiku wakiwapiga risasi watu na kuwadunga visu mbali na kuchoma nyumba zao.

No comments

Powered by Blogger.