Full-Width Version (true/false)


Serikali yamnyang'anya mkandarasi mradi
Serikali imelazimika kuingilia kati utekelezaji wa mradi mkubwa wa Maji wilayani Gairo uliokwama  kwa zaidi ya miaka nane kutokana na kutoa maji yenye chumvi kupita kiasi  na kumyang’anya mkandarasi aliyepewa kazi hiyo baada ya kushindwa kununua Mtambo wa kuchuja Chumvi. 

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr. Kebwe Stephen amesema Mradi huo umegharimu zaidi ya shilingi billion 4.1 na utekelezaji wake ulianza tangu mwaka 2010 na ulitakiwa kukamilika February 2012 lakini umeshindwa kukamilika baada ya  kutoa maji yenye chumvi kupita kiasi ambayo hayafai kwa matumizi ya binadamu.

Aidha Mhandisi huyo Heka Bulugu amesema miongoni  mwa changamoto zilizopelekea kukwama kwa mradi huo ni kukosekana kwa huduma ya umeme katika maeneo yaliyopitiwa na mradi huo kwani Mtambo wa kuchuja chumvi unatumia nishati hiyo.

Pamoja na hayo Serikali imeahidi kununua mtambo huo baada ya mkandarasi kushindwa.

No comments

Powered by Blogger.