Serikali yatoa majibu kuhusu sehemu zisizo na minara ya mawasiliano
Serikali inakusudia kuanisha maeneo ambayo hayana mvuto wa kibiashara
na kutangaza tenda kuweka minara ya simu ili wananchi waweze kupata
mawasiliano.
Hayo yamebainishwa leo, Mei 15 Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri
wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye ambapo amesema
kuwa makampuni ya simu yanafanya biashara na ili waweke minara ni lazima
eneo liwe na mvuto wa kibiashara.
“Mfuko wa mawasiliano wa wote ni Taasisi ya serikali ambayo inahusika
kupeleka mawasiliano katika vijiji vyote ambavyo ambazo hazina mvuto wa
kibiashara haya Makampuni ya simu yanafanya biashara ili yaweze kufanya
biashara sehemu moja wapo ni lazima pawe na mvuto wa kibiashara,
kuepuka serikali ilianzisha mfuko wa mawasiliano kwa wote kuhakikisha
hata zile sehemu zisizo za kibiashara zinapata mawasiliano,” Mh. Nditie.
Aidha Ntitiye alisema atafanya ziara nchi nzima katika maeneo ambayo
hayana mawasiliano haswa kwa wabunge walioleta barua ambao maeneo yao
hayana mawasiliano.
No comments