Full-Width Version (true/false)


Serikali yatoa ufafanuzi kuhusu kiasi wanacholipwa waliokufa vitani
Serikali kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa limetolea ufafanuzi juu ya mafao ya askari wanaopata ajali au kufariki wakiwa kwenye kazi ya kulinda amani nchini ya Umoja wa Mataifa, na kusema kwamba askari hao hulipwa fidia kutoka kwa Umoja wa Mataifa.

Akifafanua suala hilo Bungeni Waziri wa Ujenzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hussein Mwinyi, amesema askari hao hulipwa na Umoja wa Mataifa wenyewe na sio nchi, na wala nchi haihusiki kupanga kiasi cha fidia kinacholipwa cha Umoja wa Mataifa ambacho ni dola za Marekani elfu 70.

Waziri Mwinyi ameendelea kwa kusema licha ya mafao hayo yanayotolewa na Umoja wa Mataifa, serikali pia kupitia wizara yake hutoa pesa za mafao ambazo hulipwa kwa familia ya marehemu aliyefariki akiwa kwenye 'mision'.

"Fidia ya askari aliyeumia au kufariki akiwa kazini huwa inasimamiwa na Umoja wa Mataifa, nchi haipangi ni kiasi gani apewe. Umoja wa Mataifa inalipa dola za Marekani elfu 70 kwa askari yeyote aliyefariki akiwa anatekeleza majukumu ya Umoja wa Mataifa, pia kuna fidia zinazotolewa hapa nyumbani na wizara kwa ajili ya kulipa familia ya yule aliyepoteza uhai akiwa kazini", amesema Waziri Husein Mwinyi

Pia Waziri Mwinyi amesema pesa hizo zinapotolewa na Umoj wa Mataifa zinakuja kamili bila makato ya aina yoyote, hadi kuwafikia walengwa ambao ni familia ya marehemu.

No comments

Powered by Blogger.