Full-Width Version (true/false)


Serikali yawahakikishia waislamu kufunga mwezi mtukufu bila matatizo

Serikali ya awamu ya tano kupitia Bunge lake limewahakikisha waaumini wa dini ya kiislamu kuwa watahakikisha upatikanaji wa mafuta na Tende unakuwa wa kutosha pamoja na kuwepo bei nzuri ili waweze kula vyakula vya mafuta kwa wingi katika mwezi wa mtukufu wa Ramadhani utakaoanza siku zijazo

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage leo Mei 07, 2018 Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 23 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la Mbunge Hussein Bashe aliyetaka kusikia kauli ya serikali juu ya kuangalia uwezekano wa kufuta kodi katika uingizaji wa Tende nchini kutokana na kuwa zao hilo linatumika kwa kiasi kikubwa ndani ya mwezi wa Ramandani unaotarajiwa kuanza ndani ya mwezi huu pamoja na bei ya mafuta ya kula na sukari kuwa juu kwa kipindi kifupi.

"Sasa hivi kwenye hifadhi ya mantenki Dar es Salaam kuna CPO takribani tani 40,000 na meli zilizopo nje zina CPO tani 50,000. Kinacholeta tatizo ni kutokubaliana katika viwango vya kodi maana ukileta mafuta kwa sheria tuliyopitisha sisi watanzania tunamtoza muagizaji asilimia 10. Lakini kama nilivyowaeleza tunayo hazina ya kutosha 'Crued Oil' tani elfu tisini 90,000 kwa hiyo niwahakikishie katika mwezi mtukufu wa Ramadhani tutakwenda kufunga vizuri na tutakula vyakula vyetu vyenye mafuta ya kutosha",amesema Mwijage.

Pamoja na hayo, Waziri Mwijage ameendelea kwa kusema "suala la Tende ni jambo la kwenda kuzungumza na Waziri wa Fedha na kuna kikao tumekifanya juzi kwasababu hakikuwepo katika sheria yetu tuliyoipitisha lakini baada ya kuona tangazo kutoka nchi ya jirani ndio ikawa inazunguka. Katika vikao vilivyo rasmi na mimi nimeliona kwa hiyo tutalipeleka kwa Waziri wa Fedha ili twende kumshawishi kwenye busara hii ili kusudi katika mwezi huu Bunge lichume thawabu na nchi ichume thawabu".

Kwa upande mwingine, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema atalishughulikia suala la kodi la uwingazaji mafuta ili iweze kufahamika kama ni asilimia 10 inapaswa kutozwa na serikali au asilimia 25.

No comments

Powered by Blogger.