Full-Width Version (true/false)


Shaffih Dauda afunguka kiwango cha Dilunga Mtibwa

Tukiachana na mambo mengine Hassan Dilunga kwa sasa yupo on fire mbaya, anafunga na ku-assist. Ni nguzo ya Mtibwa kufanya vizuri msimu huu katika ligi na kombe la TFF.

Amekuwa na mfululizo mzuri wa kufunga, jana aliunga goli pekee lililoipa Mtibwa pointi tatu mbele ya wenyeji Njombe Mji ambao walikuwa wanahitaji pointi tatu kuliko kitu kingine chochote.

Aliifunga timu yake ya zamani Yanga kwenyenuwanja wa Jamhuri Morogoro, Mtibwa ikaondoka na pointi tatu lakini Dilunga ndiye aliyeipeleka Mtibwa fainali ya kombe la TFF kwa mabao yake mawili dhidi ya Stand United kwenye mchezo wa nusu fainali.

Kama umefatilia game za Mtibwa Sugar, Dilunga anachezeshwa kama namba 10 na kumfanya awe free, hana majukumu mengi zaidi ya kufanya ubunifu kutokana na kucheza karibu na goli.

Zamani alikuwa anachezeshwa kama kiungo wa kati ‘deep’ tofauti na siku hizi ambapo anacheza nyuma ya mshambuliaji halafu amepunguziwa majukumu ya kurudi nyuma kuchukua mipira na kucbezesha.

Sasa hivi anapokea mipira na kufanya kazi ya kuisambaza kwa washambuliaji lakini kwa sababu anacheza nyuma ya goli na anauwezo mzuri wa kupiga mashuti ndio maana anafunga kadiri anavyotaka.

Pongezi kwa kocha Zuberi Katwila kwa kujua kumtumia Dilunga, hakuna mahali imeandikwa mchezaji fulani ni kwa ajili ya nafasi fulani ndio maana tunamuona Shomari Kapombe anacheza nafasi ya kiungo na anafanya vizuri.

Hadi sasa Dilunga amefunga magoli matano kwenye ligi kuu Tanzania bara na magoli manne kwenye kombe la FA hivyo kwa ujumla ameshafunga magoli tisa msimu huu.

credit to shaffihdauda.co.tz

No comments

Powered by Blogger.