Full-Width Version (true/false)


Shilole Achekelea Mfungo Ndani ya Ndoa "Huu ni mfungo wa Kipekee Kwangu"

WAKATI waumini wa Dini ya Kiislam wakiendelea na Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, staa wa muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amechekelea mfungo huo ulivyo wa tofauti na miaka mingine kwake kwani yupo ndani ya ndoa.

Shilole aliiambia Za Motomoto News kwamba, katika mfungo wa mwaka huu, anaona raha mno kwani ndiyo kwa mara ya kwanza umemkuta ndani ya ndoa na amekuwa akifunga na kufanya dua na mumewe, Ashraf Uchebe tofauti na miaka mingine ambayo alikuwa hajaolewa, alikuwa akilegalega kufanya sala na kufunga.

“Huu ni mfungo wa kipekee kwangu kwani ndiyo kwanza umenikuta ndani ya ndoa, kiukweli ninajisikia raha mno ambayo sikuwahi kuipata awali,” alisema Shilole au Shishi Baby

Shilole aliwataka mastaa wa kike ambao hawajaolewa wajitahidi waolewe na waachane na kuzini kwa sababu dua zao ndipo zitakapopokelewa pia anawaombea ili wapate waume wema kama yeye alivyopata mume mwema anayemuongoza katika njia nzuri ya kumjua zaidi Mwenyezi Mungu.

No comments

Powered by Blogger.