Shilole awafungukia wanaume wanaoazima nguo
Msanii wa BongoFleva na mjasiliamali nchini Tanzania, Zuwena Mohamedy maarufu kama 'Shishi Babe' amefunguka na kuwataka baadhi ya wanaume wenye tabia ya kuvaliana au kuazima nguo hasa za ndani kuacha mara moja kwa kuwa jambo hilo sio zuri.
Shishi
Babe ametoa kauli hiyo siku za hivi karibuni wakati alipokuwa
anazungumza kwenye kipindi cha DADAZ kinachorushwa na tinga namba moja
kwa vijana EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi 6:00
mchana baada ya kuulizwa swali na waongozaji wa kipindi hicho kuwa ni
kwa nini watu wanapenda kuazima vitu na kushindwa kurudisha.
"Zamani wanawake walikuwa wanaongoza kwa kuazimana lakini
hivi sasa mpaka wanaume wanaazimana nguo mpaka za ndani. Mimi sipendi
kabisa masuala ya kuazimana vitu haswa nguo kama wanavyofanya wadada
wengine wa mjini na kama mtu akija kuniazima kitu kwangu huwa naangalia
na muda mwingine naigawa kabisa na siwezi kuichukua tena", amesema Shishi Babe.
No comments