Full-Width Version (true/false)


Shomari Kapombe apata dili la kwenda kucheza LaLiga nchini Hispania
Nyota inaendelea kumuwakia beki kiraka wa Simba, Shomari Kapombe kwani sasa taarifa zinasema anatakiwa na moja ya timu iliyopanda kucheza Ligi Kuu ya Hispania msimu ujao.
 

La Liga ni ligi kubwa Ulaya ambapo mas­taa mbalimbali wanacheza wakiwemo Lionel Messi wa Barce­lona na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.
 

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Simba, kimeeleza kuwa timu kubwa kutoka His­pania ambayo imepanda ligi kuu inamtaka Kapombe alipokuwa akiichezea Simba mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry ya Misri baada ya kuvutiwa na uwezo wake.
 

Kwa mujibu wa gazeti la Championi lilimtafuta Kapombe ili aweke wazi kuhusiana na taarifa hizo, am­bapo alisema: “Nikweli kuna mawakala zaidi ya watatu wamenipigia hivi karibuni wakini­taarifu uwepo wa timu zaidi ya tatu kunihitaji.”
 

“Wakala wa kwanza ameniambia kuna timu ya Hispania inanitaka, lakini pia zipo zingine mbili, moja kutoka Urusi na nyingine ipo Bara la Asia ambazo zote nimeshataari­fiwa kuni­hitaji, hivyo wakala wangu ameniomba nitume tu baadhi ya ‘clip’ (video) zangu ili aweze kuka­milisha dili hilo.
 

“Hii ni bahati sana kwangu kuonekana kwa muda mfupi huu ambao nimecheza Simba, japo nia yangu ningependa kuendelea kuwa hapa ili nijiweke vizuri zaidi kwani nina malengo mengi sana ambayo bado sijayafi­kia pamoja na kwamba wao wameshaona uw­ezo wangu,” alisema Kapombe.

No comments

Powered by Blogger.