Full-Width Version (true/false)


Shujaa wa Ujerumani 2014 atemwa kwenye kikosi cha kombe la Dunia

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Löw, hajajumuisha jina la shujaa wa kikosi chake kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil dhidi ya Argentina Mario Gotze.
Katika majina ya wachezaji 27 aliyoyataja leo kabla ya mchujo utakaobakiza wachezaji 23, watakaosafiri kwenda kutetea ubingwa wao huko Urusi, Low hajamtaja mshambuliaji huyo wa Borrusia Dortmund ambaye alifunga bao katika dakika za nyongeza lililoipa ubingwa Ujerumani.

Low pia ameongeza mkataba wa miaka miwili na sasa ataifundisha nchi hiyo hadi mwaka 2022. Kwa maana hiyo Low atakuwa kwenye benchi la Ujerumani kwenye fainali za EURO 2020 na Kombe la Dunia 2022.

Kikosi kamili:

Makipa: Bernd Leno (Bayer Leverkusen), Manuel Neuer (Bayern Munich), Marc-Andre ter Stegen (Barcelona), Kevin Trapp (Paris St-Germain)

Walinzi: Jerome Boateng (Bayern Munich), Matthias Ginter (Borussia Monchengladbach), Jonas Hector (Cologne), Mats Hummels (Bayern Munich), Joshua Kimmich (Bayern Munich), Marvin Plattenhardt (Hertha Berlin), Antonio Rudiger (Chelsea), Niklas Sule (Bayern Munich), Jonathan Tah (Bayer Leverkusen)

Viungo: Julian Brandt (Bayer Leverkusen), Julian Draxler (Paris St-Germain), Leon Goretska (Schalke), Ilkay Gundogan (Manchester City), Sami Khedira (Juventus), Toni Kroos (Real Madrid), Mesut Ozil (Arsenal), Sebastian Rudy (Bayern Munich), Leroy Sane (Manchester City)

Washambuliaji: Mario Gomez (Stuttgart), Thomas Muller (Bayern Munich), Nils Petersen (SC Freiburg), Marco Reus (Borussia Dortmund), Timo Werner (RB Leipzig).

No comments

Powered by Blogger.