Full-Width Version (true/false)


SIMBA, AZAM ZAIPUKUTISHA YANGA


Licha ya ku­maliza msimu kwenye nafasi ya tatu ambayo ni mbaya zaidi kuwahi ku­watokea katika miaka ya hivi karibuni, Yanga im­ekumbana na kasheshe jingine ambalo limefan­ya mambo yao kuwa ma­baya zaidi.


Simba na Azam zimea­mua kuanzia vurugu zake za usajili katika kikosi cha Yanga ambapo zote mbili zimeikomalia kwelikweli huku mastaa wakubwa wa Jangwani wakionekana kupagawa na mafungu waliyowekewa mezani.
 

Usajili rasmi unaanza Juni 15 lakini Simba na Azam zimeanza kuvuna Jangwani. Kwanza Yanga walikuwa wanamtaka Adam Salamba kutoka Lipuli, lakini juzi jioni ali­washangaza wengi baada ya kutua Simba kwa kile kilichodaiwa kuwa Yanga walishindwa kufikia dau linalotakiwa.
 

Simba wamempa Salamba Sh40milioni taslimu na jana Jumanne walimkabidhi gari ya kutembelea aina ya Crown mpya yenye thamani ya zaidi ya Sh15milioni.
 

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, limeeleza kuwa linafahamu kuwa wache­zaji muhimu wa Yanga wanaondoka na kujiunga Azam na Simba na kili­chobaki ni ishu ya muda tu kwani wameshashaw­ishika.


Wachezaji wanaotara­jiwa kuondoka ni Papy Kabamba Tshishimbi, Kelvin Yondani, Hassan Kessy na Obrey Chirwa huku Donald Ngoma yeye akiwa ameshasaini Azam, kila mmoja ataondoka kwa dau lake na sababu kubwa ni ukata na maisha magumu ndani ya Yanga ambapo hawapati sapoti yoyote kwa wadau kama awali.
 

Lakini nje ya Yanga Simba wanaweza kuwa­nasa pia, Pascal Wawa na Tafadzwa Kutinyu kutoka Singida United.
 

PAPY TSHISHIMBI:

Huyu bado ana mkata­ba wa mwaka mmoja kwa sasa, lakini Simba wamepa­nia wanamtaka na wana nia kweli, muda wowote unaweza kusikia chochote.
 

“Huwezi kua­mini hata y e y e mwenyewe a n a t o a ushirikiano m k u b w a kwa Simba na hata l e o ( j a n a ) tutawasiliana nae tena,”alisisitiza kiongozi mmoja makini wa Simba.
 

“Huyu Simba wanaweza kuwapa Yanga hata mil­ioni 100,hela ipo sasahivi, Yanga wanatafuta hela ya kusajili,”kiliongeza chanzo chetu cha uhakika.
 

Hata hivyo, imefahamika kuwa mchezaji huyo naye anataka kuondoka kwenye timu hiyo kutokana na hali ya kiuchumi kuwa mbaya hivyo anaweza kuwashawi­shi viongozi wake wakavun­ja mkataba na kujiunga na timu hiyo.
 

Tshishimbi alisaini mkataba wa miaka miwili na sasa amebakiza mwaka mmoja tu na kuna baadhi ya vitu kwenye mkataba wake ambavyo inaelezwa Yanga hawajavitimiza am­bavyo vinaweza kumruhu­su akauvunja mkataba huo.
 

KELVIN YONDANI

Awali ilikuwa inaelezwa kuwa Simba wanamtaka beki huyo lakini kibao kime­badilika na sasa anawe­za kwenda kujiunga na Azam.
 

A n a y e ­t a r a j i w a kuwa ko­cha mpya w a A z a m kuanzia msimu ujao, Hans van Pluijm amepend­e k e z a jina la beki huyo m w e n y e uwezo wa juu kuwa asajiliwe na timu hiyo.
 

H a t a hivyo, haku­na kizuizi chochote kinachom­zuia kwenda kwenye timu hiyo kwa kuwa hadi sasa yeye ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika.
 

HASSAN KESSY

Hakuna aliyekuwa a n a f i k i r i k u h u s u H a s s a n K e s s y k w e n ­d a A z am, l a k i n i m a m ­bo ya­naelezwa kuwa y a m e b a d i l i k a baada ya beki ali­yekuwa anatakiwa na timu hiyo Juma Abdul kugoma kuondoka Yanga, ndiyo wakaweka nguvu kwa Kessy am­baye naye h a n a mk a t a ­ba na timu hiyo ya Jang­wani.
 

Kessy anawadai Yanga na wala hajasaini mkataba hadi sasa, Azam wame­shazungumza naye na kuna uwezekano mkubwa akasaini wiki hii kwa kuwa kila kitu kinaonekana kuwa tayari kukamilika alisema mtu wa karibu na Kessy.
 

PASCAL WAWA

Kwa mashabiki wa soka la Tanzania wanamfahamu beki huyo kisiki raia wa Ivory Coast, lakini habari ya kushtua ni k w a m b a a n a k u j a nchini na k u s a i n i S i m b a mwaka mmoja.
 

Simba wanamtaka Wawa kwa kuwa wanafa­hamu kuwa ana uzoefu wa kimataifa na atawasaidia sana msimu ujao ambao wanaingia kwenye michua­no ya Klabu Bingwa Afrika.
 

Wawa amemalizana na timu yake ya sasa El Mer­reikh ya Sudan na ame­shafanya mazungumzo ya awali na kiongozi mmoja wa Simba na inaelezwa katika mazungumzo yao mchezaji huyo amesema anahitaji mshahara tu kwanza apige kazi bila fed­ha yoyote ya usajili.
 

Inaelezwa kuwa akiwa Sudan alikuwa anaende­lea kuwa mchezaji tege­meo kama wakati akiwa na Azam.
 

TAFADZWA KUTINYU

Habari ny­ingine njema kwa mashabiki wa Azam, ni kwamba klabu yao im­epindua meza na tayari imekamilisha usajili wa kiungo wa Singida United, Mzimbambwe Tafadzwa Kutinyu.
 

Awali uongozi wa Singi­da ulionekana kuweka ngu­mu mchezaji huyo kujiunga na Azam lakini mwenyewe alishinikiza kuwa anata­ka kuondoka na kwenda Azam.
 

Kocha Pluijm al­ishindwa kumshawi­shi kuendelea na timu ya Singida kwa kuwa timu hiyo inashiriki michuano ya kimataifa na hivyo akasema ana­kwenda Azam lakini kwa mzuka wa viongozi wa Azam walionao lolote linaweza kutokea.
 

Siyo kimataifa tu hata fedha kwa kuwa ingekuwa ni hivyo angesubiri Sing­ida wacheze na Mtibwa fainali ya Kombe la FA kwani wangeweza kupa­ta nafasi hiyo lakini yeye alisisitiza kuwa anataka kwenda Azam na inase­mekana amesajiliwa Azam kwa gharama ya dola 20 , kilisema chanzo kutoka Singida.
 

OBREY CHIRWA

S i m b a w a m e ­shasema k u p i t i a msemaji wao Haji Manara kuwa watak­wenda nchini Kenya kwenye mi­chuano ya SportPesa na jina kubwa kwenye mi­c h u a n o hiyo zaidi ya Salamba na taarifa zinasema kuwa wapo ka­ribu sana kumalizana na Chirwa ambaye mambo yake yanasimamiwa na Jo­nas Tiboroha.
 

Habari zinasema kwamba Chirwa anataka kutua Msimbazi na ana na­fasi kubwa ya kumrithi Lau­dit Mavugo ambae bado yupo Sinza, Dar es Salaam anakula bata lakini ame­shapigwa chini.
 

Hata hivyo, inaelezwa kuwa kuna vita kubwa sana kati ya Simba na Azam kuhusu mchezaji huyo.
 

Ofisa Habari wa Simba alisisitiza jana Jumanne kwamba; “Tutalipiza kila aina ya kisasi walichotu­fanyia wakati ule. Kwenye usajili tunafuata maelekezo ya Kocha lakini kuna sehe­mu fulani siasa za usajili zi­naruhusiwa, unachomeka kidogo kumuumiza mtani wako.”
 

“Nakwambia tutashtua, kuna jina moja kubwa tu­nakwenda nalo Nairobi. Nakwambia tutashtua. Hao ambao mmesha­wasikia mpaka sasa ni chamtoto,”alisisitiza Man­ara ambaye amekuwa ni mtu mwenye furaha kwa madai kwamba Yanga iliwazingua sana enzi za Mwenyekiti Yu­suf Manji.

No comments

Powered by Blogger.