Full-Width Version (true/false)


Simba imeenda Songea bila wachezaji hawa muhimu

 


Kikosi cha Simba kimeondoka jijini Dar es Salaam leo asubuhi kuelekea mjini Songea kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa ligi kuu msimu huu dhidi ya Majimaji FC.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu huu, wameondoka bila wachezaji baadhi waliocheza mchezo  wa ligi ambao walikabidhiwa kombe dhidi ya Kagera Sugar kwa ajili ya kuwapumzisha.
Nyota John Bocco, Shiza Kichuya na Emmanuel Okwi ni miongoni mwa wachezaji waliosalia Dar es Salaam huku wengi wa kikosi cha pili wakisafiri na timu kuhitimisha safari ya msimu huu.
Wachezaji hao wameamua kupumzishwa kwa ajili ya maandalizi ya baadaye ya SportPesa Super Cup inayotarajiwa kuanza mwezi Juni 2018 nchini Kenya.
Kuelekea mechi hiyo, uongozi Simba umesema hawaendi kuihurumia Majimaji bali wanaenda kuweka heshima ya kupigania matokeo.

No comments

Powered by Blogger.