Full-Width Version (true/false)


Simba: Kocha Lechantre Kama Anataka Kuondoka Tunamruhusu

BAADA ya kumaliza mkataba ndani ya kikosi cha Simba, uon­gozi wa timu hiyo umeweka wazi kwamba kama kocha wao mkuu Pierre Lechantre raia wa Ufaransa, atataka kuondoka na kwenda ku­fundisha mahali pengine basi wao watamruhusu kufanya hivyo.

Lechantre aliyeipa Simba ubingwa wa ligi kwa msimu huu amemaliza mkataba wake wa miezi sita ambapo kwa sasa amekuwa akihusishwa kutimka baada ya kuwa na ofa ya kwenda kuifundisha timu ya taifa ya Cameroon.

Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Simba, Haji Manara amesema kwamba wao hawana neno endapo Mfaransa huyo ataamua kutimka ndani ya kikosi hicho kwenda kufanya kazi sehemu nyingine kutokana na kutokuwa naye na mkataba.

“Kama kocha ataamua kuondoka ndani ya timu basi sisi kwetu tut­amruhusu kwa sababu mkataba wake wa kufanya kazi na sisi umeshamalizika baada ya ligi kumalizika na kwa kiasi kikubwa tunamshukuru kutokana na kazi ambayo ameifanya akiwa hapa kwa muda wote ambao amekaa.

“Sisi tunamshukuru kwa kile ambacho amekifanya akiwa na sisi hapa na kama akienda kufanya kazi katika timu ya taifa ya Cameroon, basi hiyo kwetu itakuwa sifa kubwa kwani ametoka hapa ndipo ameenda huko, kwa namna yoyote ile sisi tunasema kwamba tu­namshukuru kwa kile ambacho ame­kifanya na tunamtakia kila la kheri,” alisema Manara.

No comments

Powered by Blogger.