Full-Width Version (true/false)


Simba mwendo mdundo,yaichapa Ndanda 1-0
Constater wa ligi kuu Tanzania bara wekundu wa Msimbazi Simba wameendelea kukusanya point muhimu kuelekea kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa ligi kuu Soka nchini wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC kutoka Mtwara.

Kama ilivyokuwa katika mechi iliyopita dhidi ya Yanga Simba ilifanikiwa kupata bao lake dakika za mwisho za Kipindi cha Kwa baada ya mpira uliopigwa na Shomari Kapombe kumkuta Emmanuel Okwi ambaye aliwahadaa mabeki wa Ndanda FC nao wakidhani atatoa pasi akaamua kupiga shuti llililojaa wavuni umbali wa mita 20 toka katika lango la Ndanda FC.

Hilo lilikua bao lake la 20 katika msimu huu na kumfanya ndiye mwenye nafasi kubwa zaidi ya kuchukua zawadi ya mfungaji bora.

Simba sasa itahitaji pointi moja tu kufikisha pointi 66 ambazo zitawafanya kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa ligi kuu Soka Tanzania bara Kwa msimu wa mwaka 2017/2018 huku mechi inayofata Ikiwa ni ya ugenini dhidi ya timu ngumu ya Singida United.

No comments

Powered by Blogger.