Simba na Yanga sio uadui, mwanangu mwenyewe wa kumzaa ni Yanga – Haji Manara
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Haji Manara,
amefunguka kuhusu matusi anayoyapata kutoka kwa mashabiki wa Yanga.
Akiongea kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Manara amesema
anatukanwa sana na mashabiki wa Yanga mpaka imefikia hatua
wanamuunganisha kwenye magroup yao ya Whatsapp ya timu yao.
“Ninatukanwa sana, matusi mabaya ya ushamba, na wengine wananiunga hadi kwenye magroup ya whatsapp ya Yanga,” amesema Manara.
“Simba na Yanga sio uadui ni watani wa jadi. Mimi mwanangu mwenyewe wa kumzaa ni Yanga,” ameongeza.
No comments