Full-Width Version (true/false)


Simba SC na Singida United zakwama kutumia wachezaji wao waapyaKlabu za soka za Simba SC na Singida United, hazitawatumia nyota wake wapya kwenye michuano ya Sportpesa Super Cup inayotarajia kufanyika nchini Kenya kuanzia mwezi Juni. 

Kwa mujibu wa kanuni za michuano hiyo klabu hizo ambazo tayari zimeshaanza usajili wa wachezaji kwaajili ya msimu ujao, hazitapata nafasi ya kuwatumia katika michuano hiyo.

Kamati ya mashindano hayo imeweka wazi kuwa wachezaji ambao ni halali kutumika ni wale waliokuwa na timu shiriki katika michuano ya ligi zao za nyumbani. Singida United imemsajili Dany Lyanga wakati Simba imeshawasajili Adam Salamba na Marcel Kaheza.

Michuano hiyo inayoanzia hatua ya Robo Fainali, Simba SC watafungua dimba na Kariobangi Sharks Juni 3 wakati Singida United itaanza na AFC Leopards Juni 5.

Msimu uliopita Gor Mahia ilikuwa bingwa wa kwanza wa michuano hiyo baada ya kuwafunga mahasimu wao, AFC Leopard 2-1 katika fainali kwenye michuano iliyofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
 

No comments

Powered by Blogger.