Full-Width Version (true/false)


SIMBA WAJUMUIKA MSOSI WA JIONI NA WABUNGE DODOMA,Baada ya mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Dodoma Combine kumalizika Uwanja wa Jamhuri kwa sare mabao 2-2, mabingwa wapya wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2017/18 Simba SC, jana walifanyiwa hafla ya mlo wa jioni na wabunge wanaoishabikia timu hiyo.

Kikosi hicho kilifanyiwa hafla fupi na wabunge ambao wanaishabikia Simba kwa kujumuika nao katika chakula cha jioni jijini Dodoma.

Simba ipo Dodoma baada ya kuwasili jana ikitokea mjini Singida kushiriki mchezo wa ligi ambapo ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida United.

Baada ya kuwasili jijini humo jana na kujumuika katika mlo wa jioni na wabunge, kikosi hicho kimepata mwaliko wa kwenda bungeni leo kupata pongezi baada ya kufanikiwa kuwa mabingwa wa ligi.

Simba watapata wasaa wa kuhudhuria kikao cha leo katika Bunge la Jamhuri ili kupata pongezi zao baada ya kuchukua ubingwa huo wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja.

Simba watakuwa wanaweka rekodi ya kufika Bungeni ikiwa ni mara ya kwanza tangu Dodoma ipewe hadhi ya kuwa jiji.

No comments

Powered by Blogger.