Full-Width Version (true/false)


SIMBA WATANGAZA KUWAPELEKA BOCCO, KICHUYA NA OKWI KENYA ILI KUCHEZA NA EVERTON

Uongozi wa klabu ya Simba umedhamiria kufanya vema katika mashindano ya Sport Pesa Super Cup inayotarajia kuanza Juni 3 mpaka 10 mwaka huu nchini Kenya.
Kupitia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu hiyo, Said Tully, amesema kuwa awamu hii wamedhamiria kufanya vizuri hivyo hawatapeleka kikiso cha pili kama walivyofanya msimu uliopita.
Tully ameeleza kuwa Simba itaenda na kikosi kamili ambacho kimecheza mechi za ligi ili kuweka nguvu ya kupambania nafasi ya kucheza na Everton huko England.
Mjumbe huyo ameeleza kuwa watafanya hivyo na hawataonesha kuidharau michuano hiyo kama ambavyo walifanya msimu uliopita ambapo pia watani zao wa jadi Yanga nao walitumia kikosi cha pili.
Mshindi wa Kombe hilo ambalo mwaka mwaka jana lilifanyika nchini Tanzania atapata nafasi ya kucheza na klabu ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu Uingereza.

No comments

Powered by Blogger.