Full-Width Version (true/false)


SIMBA YAENDA SARE NA KOMBAINI YA DODOMAKikosi cha Simba kimeenda suluhu ya mabao 2-2 dhidi ya Combine FC ya mjini Dodoma katika mchezo wa kirafiki.

Simba ilikuwa mgeni wa mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.

Mabao ya Simba yamefungwa na Ally Shomari pamoja na Shiza Kichuya.

Simba iliwapana nafasi zaidi wachezaji wa kikosi cha pili ili kuwaweka fiti wakati kikosi hicho kikitarajia kurejea Dar es Salaam siku ya kesho.

Mabingwa hao wa ligi msimu huu wanatarajia kuwasili Dar kesho kuanza maandalizi ya mechi na Kagera itakayopigwa Uwanja wa Taifa.

No comments

Powered by Blogger.