Full-Width Version (true/false)


Simba yakabidhiwa kombe kinyonge, wachapwa mbele ya Rais Magufuli

 


Klabu ya Simba SC imekubali kichapo cha goli moja bila dhidi ya timu ya Kagera Sugar katika mechi ya kubabidhiwa kombe la VPL iliyochezeka katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Rais John Pombe Magufuli ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika mechi hiyo iliyokuwa na msisimko mkubwa kwa upande wa wekundu wa msimbazi hao kutokana na kukosa kombe hilo kwa miaka 5 mfululizo.

Akiongea akiwa uwanjani hapo kabla ya kuwakabidhi Simba SC kombe, Rais Magufuli aliipongeza kablu hiyo huku akiwataka wekundu hao kuongeza juhudi katika michezo ijayo kwani mchezo waliouonyesha mbele ya Kagera Sugar hauwezi kuwafikisha sehemu yoyote.

“Hongereni sana Simba kwa kutwaa ubingwa, wakati naambiwa nije katika mchezo huu mlikuwa ni klabu ambayo imechukua ubingwa bila kufungwa na timu yoyote, na duniani kote mlikuwa ni Simba SC pamoja na Barcelona, Jumamosi nikasikia Barcelona wamefungwa hivyo rekodi yao kuvunjwa, leo tena Simba rekodi yao imevunjwa na Kagera Sugar, hongereni sana Wanasimba,” alisema Rais Magufuli.

Aliongeza, “Nitaendelea kuwa karibu na nyie na timu yoyote ambao inaleta makombe kwa sababu napenda mafanikio na mimi pia napema michezo, kila timu itakavyochukua kombe nitajitahidi kufanya hivyo tena nataka tuanze kufanya vizuri kimataifa zaidi, Simba hongereni kwa ubingwa lakini mchezo mliouonyesha leo mbele ya Kagera hauwezi wafikisha sehemu yoyote, tuongeze juhudi kwenye hilo ili tuendelee kuitangaza nchi yetu katika michezo,”
Pia Rais Magufuli aliipongeza timu ya Serengeti Boys kwa kuchukua ubingwa ya michuano ya CECAFA mwaka 2018 huku akiwataka viongozi wa TFF kuwatumia vijana hayo katika timu ya Taifa ili kuendeleza vipaji vya soka.

No comments

Powered by Blogger.