Full-Width Version (true/false)


SIMBA YAONDOKA KUELEKEA SONGEA KUWAFARIJI MASHABIKI WAKE
Kikosi cha Simba kimeondoka asubuhi hii kuelekea Songea kwa ajili ya kuhitimisha ratiba ya mechi za Ligi Kuu dhidi ya Majimaji FC.

Mabingwa hao wapya wa ligi msimu huu wamesema hawaendi kuihurumia Majimaji ambayo ipo kwenye ipo kwenye nafasi kubwa ya kushuka daraja bali itakuwa ni ya kuwafariji mashabiki wa timu hiyo.

Kupitia Ofisa wa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema wanaenda Songea kutafuta matokeo ya pointi tatu ili kuwafariji Wanasimba kufuatia kupoteza mechi dhidi ya Kagera iliyopigwa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Manara ameeleza kipigo cha bao 1-0 walichokipata kutoka kwa Kagera na kutibua kutengeneza rekodi yao ya kushindwa kumaliza ligi bila kupoteza msimu huu kiliwachefua wengi na ili kuwafariji itabidi wakashinde mechi hiyo.

Msimamo wa ligi unaonesha Majimaji ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 24, hivyo inapaswa kupata matokeo dhidi ya Simba ili kusalia kwenye ligi, wakati huo ikiomba Ndanda wafungwe na Stand United katika mchezo uliosalia.

No comments

Powered by Blogger.