Full-Width Version (true/false)


Simba yasajili straika huyu kutoka Majimaji FC

Kabla ya hata ya Ligi Kuu Bara kumalizika taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Simba tayari wameshamalizana na nyota wa Majimaji FC, Marcel Kaheza kwa kusaini naye mkataba wa awali wa miaka miwili.


Kaheza ambaye aliwahi kuichezea Simba B na kikosi cha kwanza kisha kuchukuliwa kwa mkopo na Majimaji na baadaye baadaye kumsajili, ameonesha kiwango kikubwa msimu huu kwa kufunga idadi ya mabao 13 akiachwa na Okwi aliyefikisha 20.


Mbali na idadi hiyo ya mabao, Mshambuliaji huyo amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara kwa mwezi Aprili 2018. 


Kaheza alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, John Bocco na Emmanuel Okwi wote wa Simba ya Dar es Salaam katika uchambuzi uliofanywa wiki hii na kamati ya tuzo hizo.
 

Wakati Majimaji FC ikiwa inajiandaa kucheza na Simba Jumatatu ya wiki ijayo, inaelezwa mchezaji huyo hatokuwa sehemu ya kikosi kutokana na kusajiliwa na Simba.

No comments

Powered by Blogger.