Full-Width Version (true/false)


Simba yatangaza mechi ya kusherehekea ubingwaMabingwa wapya wa ligi kuu soka Tanzania bara klabu ya soka ya Simba, imetangaza mechi ya kirafiki dhidi ya Dodoma FC ikiwa ni maalum kwa kusherehekea ubingwa wao na wakazi wa jiji la Dodoma. 
Simba ambayo kwasasa ipo Singida kucheza mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya wenyeji Singida United, baada ya mchezo huo kikosi kitasafiri kwenda Dodoma ambako kesjo Jumapili ktacheza na mabingwa wa mkoa huo Dodoma FC.

Mbali na mechi hiyo ya kirafiki, Simba itaendelea kusalia jijini humo hadi jumatatu asubuhi ambapo kikosi kitakwenda Bungeni baada ya kupokea mwaliko maalum wa kwenda kutambulisha ubingwa wao mbele ya wabunge.
Baadae Jumatatu jioni kikosi kamili cha timu hiyo kitarejea jijini Dar es salaam kwaajili ya ratiba zingine za kufurahi ubingwa pamoja na maandalizi ya mechi zao mbili za mwisho.

Simba kwasasa ina alama 65 kwenye mechi 27 ambazo haziwezi kufikiwa na Azam FC yenye alama 52 kwenye mechi 28 wala Yanga yenye alama 48 kwenye mechi 25.

No comments

Powered by Blogger.