Full-Width Version (true/false)


Simba yatoa ratiba yake ya kusherehekea UbingwaZikiwa zimebakia siku chache kwa Klabu ya Simba kukabidhiwa kikombe chao rasmi cha ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara 2017/18, uongozi wa wekundu wa Msimbazi wamewataka mashabiki wao kuwa na utulivu kwa kuwa wanapanga ratiba kamili ya namna ya kupokea na kusherehekea kikombe hicho. 

Hayo yamewekwa wazi na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara mara baada ya timu yake kujihakikishia ubingwa wa mnono kwa kuendelea kutoa kipigo kwa kila mchezo watakao kuwa wanacheza.

"Hivi sasa tupo katika maandalizi ya mwisho kabisa ya kukabidhiwa kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara ambalo tulikuwa tuna litafuta kwa miaka mitano mfululizo. Sherehe zitaanza leo jijini Dodoma kwa kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Dodoma Combine, halafu saa 1 jioni tumealikwa 'dinner' na wabunge wanaoshabikia klabu ya Simba bila ya shaka watakuwa wanaongozwa na Spika wa Bunge Job Ndugai", amesema Manara.

Pamoja na hayo, Manara ameendelea kwa kusema "siku ya Jumatatu tutakwenda kutembelea viwanja vya Bunge na klabu ya simba kwa maana timu itatambulishwa rasmi na baada ya hapo tutakuwa tunaiyanza safari ya kuelekea Dar es salaam na kuanzia wiki hiyo kabla ya kukabidhiwa kombe nitaweleza mtiririko mzima wa sherehe zenyewe kabla ya kukabidhiwa kombe Mei 20".

Simba kwasasa ina alama 65 kwenye mechi 27 ambazo haziwezi kufikiwa na Azam FC yenye alama 52 kwenye mechi 28 wala Yanga yenye alama 48 kwenye mechi 25.

No comments

Powered by Blogger.