Full-Width Version (true/false)


SIMBA YAWASILI DAR ES SALAAM USIKU, UONGOZI WATAMBA TIMU HAITAPOAKikosi cha Simba kimewasili usiku wa jana jijini Dar es Salaam kikitokea jijini Dodoma kufuatia mwaliko wa Spika wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai aliyekialika Bungeni.

Simba walipata nafasi hiyo wakiwa wanatokea Singida kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Singida United ambapo walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mwaliko huo wa Bungeni ulikuwa ni maalum kupata pongezi za kuchukua ubingwa kufuatia kuukosa kwa muda mrefu ambao ni takribani miaka mitano.

Wakati kikosi hicho kikiwa safarini kurejea Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara, alisema hawawezi kupokea na sasa wanajipanga dhidi ya Kagera.

Simba itakutana na Kagera wikiendi hii kwenye Uwanja wa Taifa kucheza mechi ya kukamilisha ratiba na huku wakieleza lengo lao ni kuchukua ubingwa bila kufungwa.

No comments

Powered by Blogger.