Full-Width Version (true/false)


Simjui Young Tusso -Juma Nature
Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva na anayeheshimika na wengi, Juma Kassim Nature amesema kuwa hana taarifa kuwa Temeke kuna Mfalme zaidi yake. 
Nature ametoa kauli hiyo kupitia eNewz ya East Africa Televisheni kuwa endapo kuna msanii yeyote kutoka Temeke anajiita Mfalme basi atakuwa haifahamu historia ya sehemu hiyo.

“Mimi siwezi kuzungumzia habari hizo maana simjui hata huyo msanii, kama anajiita Mfalme sawa yeye Mfalme na ukiona mtu ananizungumzia basi ujue hanijui na hajui historia mimi ni ‘Legendary’ wa Temeke hakuna asiye nifahamu”, amesema Nature

Hivi karibuni msanii Young Tuso alinukuliwa akisema kwamba Juma Nature hana sifa za kuwa Mfalme wa Temeke bali yeye ndiye, kwani muda wote aliokaa kwenye game ndio jina analotumia.
Mtazame hapa chini Juma Nature akifunguka zaidi ..

No comments

Powered by Blogger.