Full-Width Version (true/false)


Singida United hatiani kushtakiwaUongozi wa timu ya JKU ya Visiwani Zanzibar umetishia kuishtaki Singida United kwa kumsainisha kiungo wao Feisal Salum ambaye bado wana mkataba naye mrefu. 

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Sadu Judu na kusema endapo itabainika Singida imemsainisha kiungo huyo wataishitaki huku akidai mchezahi huyo amebakisha miaka miwili katika mkataba wake hivyo kikanuni hawezi kusajiliwa na timu nyingine bila ya kufuatwa utaratibu ukiwemo wa kuvunjwa mkataba huo.

"Tumesikia taarifa kuwa Singida imemsainisha kiungo wetu Feisal Salum lakini wamefanya jambo ambalo sio zuri kwa kuwa mchezaji bado ana mkataba mrefu wa miaka mitatu. Nadhani Singida ilipaswa kutufuata na kukaa chini kuangalia tunafanyaje juu ya usajili wake lakini wakileta ubabe wasitulaumu kwa kitakacho watokea," amesema Judu.

Kipaji cha Feisal kilionekana vizuri katika michuano ya 'Cecafa Challenge' iliyofanyika nchini Kenya akiwa na timu ya Zanzibar Heroes iliyoingia hadi fainali mwezi Novemba mwaka 2017.

No comments

Powered by Blogger.