Full-Width Version (true/false)


SINGIDA UNITED WAIBUKA NA JAMBO JIPYA KUHUSIANA NA KUMSAINI KOCHA MPYABaada ya kuelezwa kuwa tayari umeshamalizana na aliyekuwa kocha wa Mbao FC, Etienne Ndayiragije, uongozi wa Singida United umeibuka tena na kusema bado hawajamalizana naye.

Mkurugenzi wa klabu hiyo Festo Sanga, amesema kuwa uwepo wa taarifa hizo kuwa hazina ukweli wowote na badala yake wanafanya mazungumzo na kocha ambaye ataweza kuisaidia timu kiuhakika.

Sanga amesema tayari wanaendelea na mazungumzo kwa ajili ya kumpataka Mwalimu mpya atakayerithi mikoba ya Hans van der Pluijm ambaye ataondoka baada ya mechi za msimu huu kumalizika.

Licha ya kauli hiyo ya Sanga, taarifa zilizo chini ya kapeti alizozikanusha zinasema tayari Singida wameshamalizana na Mrundi huyo kuitumikia Mbao FC.

Ujio wa taarifa za Ndayiragije umekuja ikiwa kikosi hicho kinajiandaa na mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Mtibwa Sugar, utakaopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha, Juni 2 2018.

No comments

Powered by Blogger.