Full-Width Version (true/false)


Singida United yampokea nyota wa kimataifa

Baada ya kuwa nje ya timu kwa zaidi ya miezi mitano, hatimaye nyota wa kimataifa wa Singida United na timu ya taifa ya Zimbambwe Elisha Muroiwa amerejea nchini tayari kwa kuitumikia timu yake.
Nyota huyo alilazimika kwenda kwao mwezi Desemba 2017 kutokana na matatizo ya kifamilia ambapo alipata ruhusa na baraka za timu lakini baada ya kushughulikia na kumaliza amerejea.

Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amethibitisha kuwa nyota huyo amerejea akiwa kamili kuichezea Singida United ambayo inajiandaa na fainali ya Kombe la shirikisho nchini dhidi ya Mtibwa Sugar.


Elisha Muroiwa aliiongoza timu ya taifa ya Zimbabwe kwenye michuano  ya AFCON 2017 nchini Gabon. Singida United inashika nafasi ya 5 ikiwa na alama 44 kwenye mechi zake 29 ligi kuu soka Tanzania bara.

Mbali na Muroiwa pia nyota mwingine wa timu hiyo Dany Lyanga ambaye alikuwa nje ya uwanja kutokana na usajili wake kushindwa kukamilika kwenye dirisha dogo, ameungana na timu hiyo tayari kwa maandalizi ya msimu ujao ambapo usajili wake utakamilika kwenye dirisha kubwa mwezi Julai.
 

No comments

Powered by Blogger.