Full-Width Version (true/false)


SINGIDA UNITED YATANGAZA VITA KALI NA SIMBA KUELEKEA JUMAMOSI

Uongozi wa klabu ya Singida United kupitia Mkurungenzi wake, Festo Sanga, umetamba kuvunja rekodi ya Simba kutopoteza mechi hata moja msimu huu.
Kikosi cha Singida kitakuwa kinaikaribisha Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania utakaopigwa Jumamosi ya Mei 12 2018 kwenye Uwanja wa Namfua, mjini Singida.
Sanga ameeleza kuwa Simba wasitegemee mteremko kwenye mechi hiyo kutokana na namna wanavyozidi kujipanga hivi sasa kuelekea mtanange huo.
Mkurugenzi huyo anaamini Singida italipiza kisasi walichokipata katika mchezo wa raundi ya jijini Dar es Salaam.
Singida itakuwa inaikaribisha Simba ikiwa ina kumbukumbu ya kulala kwa jumla ya mabao 4-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kwenye Uwanja wa Taifa jijini dar es Salaam uliopigwa January 18.
Vinara Simba watakuwa wanahitaji alama moja pekee kwenye mchezo huo ili kutangaza kubeba ubingwa baada ya kuukosa kwa takribani miaka mitano.

No comments

Powered by Blogger.