Full-Width Version (true/false)


SINGIDA WATHIBITISHA KUACHANA NA KOCHA HANS, SASA WANAMSAKA MBADALA WAKE


Uongozi wa Singida United umetangaza kuachana rasmi na Kocha wake, Mholanzi, Hans van der Plujim baada ya kukitumikia kikosi chao kwa msimu mmoja pekee.

Kupitia Mkurugenzi wa klabu hiyo, Festo Sanga, amesema kuwa wamefikia makubaliano ya kuagana na kocha huyo ambaye ameiwezesha timu hiyo kufika fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo itacheza dhidi ya Mtibwa Sugar.

Sanga ameeleza kuwa wataachana na Plujim mara baada ya msimu wa ligi kumalizika na sasa wapo katika mipango ya kutafuta Kocha mwingine.

Ikumbukwe Pluijim alijiunga na Singida United akitokea Yanga wakati huo akiwa Mkurugenzi wa benchi la ufundi huku George Lwandamina akiwa Kocha Mkuu.

Sanga ameshindwa kutaja ni kocha wa aina ipi wanamuhitaji kuchukua mikoba ya Pluijim kama atakuwa wa hapa Tanzania au nje ya nchi.

No comments

Powered by Blogger.