Full-Width Version (true/false)


Siri yafichuka kuondoka kwa Rooney

 Baada ya kuripotiwa kuwa nyota wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya England Wayne Rooney kuwa anaondoka kwenye klabu ya Everton mwisho wa msimu huu,  imeelezwa kuwa ni kutokana na ugomvi na kocha Sam Allardyce. 
Magazeti ya michezo nchini England, leo yameripoti kuwa Rooney ameishinikiza Everton kumwondoa kocha Sam na kama hawatafanya hivyo basi yeye ataondoka ili kumpisha kocha huyo ambaye.

Rooney alirejea Everton msimu huu akitokea Manchester United ambako alicheza kwa mafanikio kutoka mwaka 2004 hadi 2017. Ikumbukwe kuwa Everton ndio sehemu aliyoanzia maisha ya soka kabla ya kutua Man United.


Wakala wa Rooney  yupo nchini Marekani kumalizia hatua za mwisho kukamilisha uhamisho huo wa mkongwe huyo kuelekea katika klabu ya DC United inayoshiriki ligi kuu ya Marekani (MLS).

Kwa upande wake kocha wa Manchester United Jose Mourinho aliyemfundisha Rooney kwa msimu mmoja amesema maisha ya soka ya Rooney ndani ya England yameenda vizuri hivyo ni haki yake kubadili uelekeo.

No comments

Powered by Blogger.